Sarah Kaisi a.k.a akiwa na Producer maarufu nchini Joachim Kimaryo a.k.a Master J
Friday, August 8, 2014
Mjue Msanii Wako - Ambwene Yesaya (AY)
Ambwene Yesaya ni mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye anajulikana zaidi kwa jina la muziki kama AY. AY pia anajulikana kwa jina la Mzee wa Commercial.
AY alizaliwa mnamo tarehe 5, July, mwaka 1981 huko Mtwara. Inasemekana kuwa AY alianza muziki akiwa ni kijana mdogo wa miaka 10 tu.
Mwaka 1996 akiwa bado anasoma sekondari, AY akiwa na marafiki zake wawili waliunda kundi la muziki lililojulikana kama S.O.G na walitoa albam yao ya kwanza mwaka 2000.
AY pia alikuwa ni mmojawapo wa member wa kundi la East Coast alilojiunga nalo baada ya kutoka S.O.G
AY aliamua kuanza kuimba akiwa mwanamuziki wa kujitegemea bila ya kuwepo kwenye kundi lolote (solo artist) mnamo mwaka 2002.
AY ameshatoa albam kadhaa zikiwemo Raha Kamili na Hisia Zangu.
AY akiwa na rafiki yake na mwanamuziki mwenzake Hamisi Mwinjuma (Mwana Fa)
AY akiwa na P-Square
AY akipokea mojawapo ya tuzo alizowahi kupata kwenye Kili Tanzania Music Awards
AY akiwa na tuzo yake ya Channel O aliyoipata nchini Africa Kusini November 2012.
AY akiwa na mojawapo ya tuzo zake enzi hizo
Harusi za wasanii Bongo - Pastor Emmanuel Myamba
Muigizaji wa filamu za Kibongo Emmanuel Myamba ambaye mara nyingi amekuwa akiigiza kama Mchungaji na hivyo kujulikana zaidi kwa jina la Pastor Myamba alifunga ndoa na mke wake Praxeda Kasela siku ya Jumamosi ya tarehe 2 August mwaka 2014 huko Zanzibar.
Pastor Emmanuel Myamba akiwa na mkewe Praxeda Kasela
Pastor Emmanuel Myamba akiwa na mkewe Praxeda Kasela
Pastor Emmanuel Myamba na mkewe Praxeda Kasela wakionyesha vyeti vya ndoa
Pastor Emmanuel Myamba na mkewe Praxeda Kasela wakiwa wameshikilia Biblia
Pastor Emmanuel Myamba na mkewe Praxeda Kasela wakionyesha pete zao za ndoa
Pastor Emmanuel Myamba na mkewe Praxeda Kasela wakiwa na wasimamizi wao
Pastor Emmanuel Myamba na mkewe Praxeda Kasela pamoja na wasanii wenzake wa Bongo movie, Thea (wa kwanza kushoto) na zawadi (wa pili kulia)
Pastor Emmanuel Myamba na mkewe Praxeda Kasela wakionyesha zawadi waliyopewa na Kamati ya Harusi
Monday, March 24, 2014
Mjue Msanii Wako - Marlaw
Msanii Marlow akiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Marlaw (kushoto) akiwa na msanii mwenzake wa Bongo Fleva Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz
Mjue Msanii Wako - Professor Jay
Professor Jay ambaye jina lake halisi ni Joseph Haule ni mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye anaimba sana nyimbo za Hip Hop.
Professor Jay alizaliwa tarehe 29 mwezi wa 12 mwaka 1975.
Professor Jay alianza muziki mwaka 1994 akiwa mmoja wa memba kwenye kundi la Hard Blasters ambalo lilikuwa likijulikana sana na kibao chao cha Chemsha Bongo, wakati huo Professor Jay akitumia jina la Nigga J.
Alianza kuimba mwenyewe akiwa msanii anayejitegemea mwaka 2001, na ametoa nyimbo nyingi kali kama vile Nikusaidieje, Zali la Mentali, Piga Makofi, Ndio Mzee, Ndivyo Sivyo n.k
Mjue Msanii Wako - Juma Nature
Juma Nature ambaye pia anajulikana kama Sir Nature ni msanii wa Bongo fleva ambaye anaimba sana nyimbo za hip hop.
Juma Nature ambaye jina lake halisi ni Juma Kassim Kiroboto alizaliwa mwaka 1980.
Juma Nature ndiye alikuwa ni muanzilishi wa kundi la muziki lililokuwa likijulikana sana la Wanaume Family na maskani yake yakiwa Temeke jijini Dar es salaam.
Mwezi wa 11 mwaka 2006 kundi la Wanaume Family liligawanyika na Juma Nature alijitoa kutoka kwenye kundi hilo akiwa na baadhi ya wasanii wachache kutoka kwenye kundi hilo la Wanaume Family na kuanzisha kundi lingine la Wanaume Halisi ambalo linavuma mpaka sasa.
Juma Nature na mke wake Pili, siku ya harusi yao
Juma Nature na Lady Jaydee
Juma Nature (kushoto) akiwa na msanii mwenzake Mh. Temba (kulia)
Monday, February 17, 2014
Mjue Msanii wako - Bahati Bukuku
Bahati Bukuku ni mwanamuziki wa nyimbo za injili.
Bahati Bukuku akiwa na Rose Muhando (katikati) na John Shabani (kulia)
Bahati Bukuku akiwa na msanii wa orijino Komedi Masanja mkandamizaji
Bahati Bukuku akiwa na muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando
Bahati Bukuku akiwa na mwanamuziki mwenzake wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege
Dunia Haina Huruma - Bahati Bukuku
Wewe ni Mungu - Bahati Bukuku
Waraka - Bahati Bukuku
Mapito - Bahati Bukuku
Lazima Usamehe - Bahati Bukuku
Mjue Msanii wako - Rose Ndauka
Rose Ndauka ni msanii, mwandishi, muongozaji wa Filamu Tanzania na pia ni mmiliki wa kampuni ya filamu ya Ndauka Entertainment. Rose Ndauka amezaliwa tarehe 7 mwezi wa 10 mwaka 1989 katika jiji la Dar es salaam. Rose alisoma mpaka form six katika shule ya Zanaki jijini Dar es salaam mwaka 2008.
Rose Ndauka alianza kuigiza rasmi mnamo mwaka 2007 kwenye filamU inayoitwa Swahiba ambapo aliigiza kama Aisha. Baada ya filamu hiyo Rose alipata nafasi ya kuigiza katika filamu mbalimbali kama vile Mahabuba, Solemba, Deception, Lost Adam n.k
Mwaka 2010 Rose Ndauka alifungua kampuni yake mwenyewe ya filamu inayoitwa Ndauka Entertainment, ambapo ameshatoa filamu mbili za Bad Girl na The Diary kupitia kampuni yake hiyo.
Rose Ndauka ana mchumba ambaye ni msanii wa Bongo flava aitwaye Malick Bandawe ambaye alikuwa anawakilisha kundi la TNG Squad kutoka Tanga. Rose na Malick Bandawe wamebarikiwa kupata mtoto mmoja anayeitwa Naveen Bandawe.
Rose Ndauka alianza kuigiza rasmi mnamo mwaka 2007 kwenye filamU inayoitwa Swahiba ambapo aliigiza kama Aisha. Baada ya filamu hiyo Rose alipata nafasi ya kuigiza katika filamu mbalimbali kama vile Mahabuba, Solemba, Deception, Lost Adam n.k
Mwaka 2010 Rose Ndauka alifungua kampuni yake mwenyewe ya filamu inayoitwa Ndauka Entertainment, ambapo ameshatoa filamu mbili za Bad Girl na The Diary kupitia kampuni yake hiyo.
Rose Ndauka ana mchumba ambaye ni msanii wa Bongo flava aitwaye Malick Bandawe ambaye alikuwa anawakilisha kundi la TNG Squad kutoka Tanga. Rose na Malick Bandawe wamebarikiwa kupata mtoto mmoja anayeitwa Naveen Bandawe.
Rose Ndauka akiwa na mchumba wake Malick Bandawe
Rose Ndauka akiwa na mchumba wake Malick Bandawe
Rose Ndauka akiwa na mchumba wake Malick Bandawe na mtoto wao Naveen Bandawe
Rose Ndauka akiwa na mwanae Naveen Bandawe
Rose Ndauka akiwa na mwanae Naveen Bandawe
Subscribe to:
Posts (Atom)