Ambwene Yesaya ni mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye anajulikana zaidi kwa jina la muziki kama AY. AY pia anajulikana kwa jina la Mzee wa Commercial.
AY alizaliwa mnamo tarehe 5, July, mwaka 1981 huko Mtwara. Inasemekana kuwa AY alianza muziki akiwa ni kijana mdogo wa miaka 10 tu.
Mwaka 1996 akiwa bado anasoma sekondari, AY akiwa na marafiki zake wawili waliunda kundi la muziki lililojulikana kama S.O.G na walitoa albam yao ya kwanza mwaka 2000.
AY pia alikuwa ni mmojawapo wa member wa kundi la East Coast alilojiunga nalo baada ya kutoka S.O.G
AY aliamua kuanza kuimba akiwa mwanamuziki wa kujitegemea bila ya kuwepo kwenye kundi lolote (solo artist) mnamo mwaka 2002.
AY ameshatoa albam kadhaa zikiwemo Raha Kamili na Hisia Zangu.
AY akiwa na rafiki yake na mwanamuziki mwenzake Hamisi Mwinjuma (Mwana Fa)
AY akiwa na P-Square
AY akipokea mojawapo ya tuzo alizowahi kupata kwenye Kili Tanzania Music Awards
AY akiwa na tuzo yake ya Channel O aliyoipata nchini Africa Kusini November 2012.
AY akiwa na mojawapo ya tuzo zake enzi hizo
No comments:
Post a Comment