Juma Nature ambaye pia anajulikana kama Sir Nature ni msanii wa Bongo fleva ambaye anaimba sana nyimbo za hip hop.
Juma Nature ambaye jina lake halisi ni Juma Kassim Kiroboto alizaliwa mwaka 1980.
Juma Nature ndiye alikuwa ni muanzilishi wa kundi la muziki lililokuwa likijulikana sana la Wanaume Family na maskani yake yakiwa Temeke jijini Dar es salaam.
Mwezi wa 11 mwaka 2006 kundi la Wanaume Family liligawanyika na Juma Nature alijitoa kutoka kwenye kundi hilo akiwa na baadhi ya wasanii wachache kutoka kwenye kundi hilo la Wanaume Family na kuanzisha kundi lingine la Wanaume Halisi ambalo linavuma mpaka sasa.
Juma Nature na mke wake Pili, siku ya harusi yao
Juma Nature na Lady Jaydee
Juma Nature (kushoto) akiwa na msanii mwenzake Mh. Temba (kulia)