Mnamo tarehe 30 June mwaka 2012, Wasanii wa Bongo Movies wakiongozwa na mwenyekiti wao wa wakati huo Jackob Steven "JB" walitembelea hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga na kujionea hali halisi ya uhaba wa vyandarua katika baadhi ya wodi na kukabidhi msaada wa vyandarua kwa hisani ya kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Tanzania (Bongo Movie) lililozinduliwa June 30, 2012 kwenye viwanja wa Tangamano jijini Tanga. Walikabidhi msaada huo wa vyandarua ikiwa ni sehemu ya kupiga vita ugonjwa wa malaria unaopoteza maisha ya watanzania wengi katika maeneo mbalimbali nchini.
Mwenyekiti wa wasanii wa Bongo Movie wa wakati huo Jacob Steven "JB" akikabidhi msaada wa vyandarua kwa muuguzi msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga ambaye pia ni mwakilishi wa hospitali hiyo Bi Halima Msengi (kushoto).
Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na mwenyekiti wao wa wakati huo Jacob Steven "JB" wakiwa kwenye picha ya pamoja na Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga Bi Halima Msengi.
Msanii wa Bongo Movie, Mayasa Mrisho anayejulikana kama "Maya" akikabidhi chandarua kwa mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali ya Bombo, Tanga.
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa wamezunguka kitanda cha mmoja wa kinamama ambaye amejifungua watoto mapacha katika wodi ya wazazi hospitali ya Bombo jijini Tanga.
Wasanii wa Bongo Movie wakisaidia kufunga chandarua katika kitanda cha mmoja wa wagonjwa katika hospitali ya Bombo jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment