Lucas Lazaro Mhuvile ambaye anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii la Joti, ni muigizaji wa kundi la Orijino Komedi lililokua likijulikana kama Ze Comedy zamani ambapo michezo yake huonyeshwa kwenye televisheni ya TBC1.
Joti amezaliwa tarehe 9 Julai mwaka 1982, katika mkoa wa Morogoro wilaya ya Ulanga katika kijiji cha Biro.
Joti ni msanii mwenye kipaji kikubwa sana, kwani ana uwezo wa kucheza kama mwanamke, mzee kikongwe, mtoto n.k.
Joti alipitia vikundi kadhaa vya maigizo kabla ya kujiunga na kundi lake la Ze Comedy zamani na sasa orijino Komedi analofanyia kazi kwasasa. Mwaka 2000 mpaka 2001 Joti alikuwa mwigizaji katika kundi la Nyepenyo, baadaye mwaka 2001 mpaka 2002 alijiunga na kundi lingine la Sun Rise na mwaka 2002 mpaka 2003 alikuwepo kwenye kundi la Nyota Ensemble.
Joti pia anajulikana kwa majina mengine kama Hami Jay, Da Kiboga, Mzee Simbawanga, Asha Ngedere, Andunje na Joti Mdebwedo.
Joti akiwa na msanii Sandra
Joti akiwa na mtangazaji wa Clouds FM Zamaradi Mketema
Joti akiwa na mtangazaji wa Clouds FM Zamaradi Mketema
Joti akiwa na wasanii wenzake wa Orijino Komedi, kutoka kushoto ni: Joti, Wakuvanga, Mpoki, Masanja Mkandamizaji, na Mac-Regan
Joti akiwa kwenye shughuli zake za usanii