Ndumbangwe Misayo ambaye anajulikana sana kwa jina la uigizaji la Thea, ni mtoto wa kwanza katika familia ya Matilda Misayo na Gaudence Urassa. Thea alizaliwa mwaka 1982 mkoani Shinyanga kabla ya kuhamia Dar es salaam na wazazi wake, ambako alipata elimu ya msingi katika shule ya Mapambano, Sinza, na baadaye kujiunga na sekondari ya Zanaki, alikosoma hadi kidato cha Tatu kabla ya kuhamia Greens Victoria, alikohitimu kidato cha nne mwaka 2001.
Thea alijiunga na kikundi cha Mambo Hayo akiwa kidato cha kwanza tu, hata hivyo baada ya kundi la Mambo hayo kusambaratika Thea alihamia Kaole.
Baadhi ya filamu alizocheza hadi sasa ni Dadaz, Ukungu, Dunia Yangu, Revenge, Sigito, Tone la Damu, Why Me, Solemba, Born to Suffer, Simanzi ya Moyo, Trip to America, Out of Love na Bed Rest.
Thea ni mshindi wa tuzo ya vinara mwaka 2008 kama mwigizaji bora wa kike pia ni mama wa mtoto mmoja wa kiume.
Ndumbangwe Misayo a.k.a Thea akiwa na mume wake Mike Sangu siku ya harusi yao
No comments:
Post a Comment