Msanii wa wiki

Msanii wa wiki
Msanii wa wiki - Aunt Ezekiel

Tangazo

Tangazo 2

Friday, July 5, 2013

Wasanii wa Bongo na Tattoo

Irene Uwoya msanii wa Bongo movies akiwa amejichora tattoo ya nyayo za mtoto na jina la mwanae kuonyesha upendo kwa mtoto wake Krish.


Msanii Kajala wa Bongo movies akiwa amejichora tattoo ya jina la Wema kuonyesha shukrani yake kwa mwanadada huyo (Wema Sepetu) ambaye ni miss Tanzania wa 2006 na pia ni msanii wa filamu baada ya kumuokoa kwa kumtolea faini ya shilingi milioni 13 za Tanzania asiende jela kwa kifungo cha miaka mitano alichokuwa amehukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kushirikiana na mumewe Faraja Chambo kuuza nyumba iliyozuiwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU). 


Miss Tanzania 2006 na msanii Wema Sepetu akiwa amejichora tattoo yenye maneno ya kichina kuanzia shingoni mpaka mgongoni. Wema amebainisha kuwa maneno hayo ya kichina yana maana ya "Potential" kwa lugha ya kiingereza. Wema Sepetu anayo pia tattoo nyingine shingoni.


Msanii Jacky wa Chuzi akionyesha tattoo zilizoko mwilini mwake. Jacky wa Chuzi amebainisha kuwa, anazo tattoo sita, hizo tatu zinazo onekana, nyingine moja iko mguuni inaonekana pia, na mbili amefichua ya kwamba ziko kwenye maeneo yasiyoweza kuonekana.


Malick Bandawe ambaye ni mchumba wa msanii wa filamu Rose Ndauka akiwa amejichora tattoo kwenye bega lake kudhihirisha mapenzi ya dhati aliyonayo kwa mchumba wake huyo.

No comments:

Post a Comment